Tuesday, September 27, 2011
WAIGIZAJI WALE WALE KATIKA FILAMU BONGO KWANINI?
Nashukuru kwa mchango wako ndugu yangu tuko pamoja umeechangia jambo muhimu sana katika hatua ya uandaaji wa filamu (casts)au waigizaji kwa tafsiri ya kawaida, uigizaji ni taaluma wenzetu wanaenda chuoni na kusomea uigizaji tu wanajikita huko na ili uwe muigizaji mzuri lazima ujue nini utafanya utakapokuwa katika scene fulani,tabia yako,muonekano wa mwili,jinsi unavyotumia viungo vya mwili,muonekano wa uso kwa hisia mbalimbali haya yote yatakufanya uvae uhusika kama inavyotakiwa kutokana na script au hadithi ya hiyo filamu.
Ni kazi ya director(muongozaji) na muandaaji(producer) kuchagua nimuigizaji gani anafaa katika kwa scene fulani, hatua hii inaitwa casting session au audition kwa msanii mwenyewe.
kuhusu swala la waigizaji wale wale kuonekana katika filamu kama ulivyosema (fixed characters)
nitakujibu kwa ifuatavyo...
Fani ya filamu na uigizaji umechagizwa sana na maigizo yanayoendelea kuonyeshwa na hasa yale ya miaka ya nyuma na ndio hapo waigizaji maarufu walipoibuka na kujipatia majina, waigizaji hawa hawa ndiyo leo hii wameingia katika uandaaji na uongozaji wa filamu ikiwemo na kushiriki katika filamu zao na ndiyo maana hata leo wanajulikana kutokana na majina yao na uhusika waliocheza katika maigizo yao nasi ajabu filamu zao hizo hizo wakiendelea kushirikiana waigizaji wale wale kwa wanachoamini majina yao yanawabeba na inakuwa vigumu msanii asiyenajina kupata nafasi hata kama anauwezo mkubwa katika uigizaji kuliko huyo msanii mwenyewe maarufu.
Wakati mmmoja nilipata kuzungumza na msaidizi muongozaji(assistant director) katika filamu ya Nyakwesi yeye alipata kuniambia waigizaji ni wale wale kutokana na kuibuka kwa kampuni ambazo zinasambaza kazi hizi za wasanii ikiwemo na hata kuandaa filamu wanachoamini wasanii hawa wenye majina tayari ni keki kwa biashara kwa maana watafanya kazi hizo kuuzika kwa mantiki ya matakwa ya kibiashara.
Swala la kuuza sura niulimbukeni tu nasi ajabu muigizaji huyu huyu kumsikia katika redio au hata kumuona katika televisheni akijinadi kuvaa vichupi kwake ni sawa tu na hata vyombo vya habari vinatupeleka huko utasikia mtangazaji anamuuliza muigizaji huyo eti nasikia unatembea na fulani? au eti sijui umegombana na nani watangazji wetu hovyo kabisa.
Tunahitaji sana kubadilika kufikia mahala ambapo tunataka kwenda katika tansia hii ya filamu na uigizaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment