Namshukuru mungu kwa kunipa afya njema nakushukuru na wewe unayesoma mahala hapa siku chache zilizopita nili post katika wall yangu juu ya mji wa Mwanza na uzuri wake kama location kwa watengeneza filamu.
Leo nitazungumzia historia fupi ya filamu,hatua za uzalishaji filamu na jinsi unavyoweza kujifunza kuhusu filamu
Filamu ni picha zinazotembea(motion pictures) ambazo zinarekodiwa katika jamii fulanii kuelezea tamaduni na mila za jamii hizo hurekodiwa kwa kifaa maalum(camera) na hupitia hatua mbalimbali kabla haijafikia katika uzalishaji.
Tunaona picha hizo sisi kama watazamaji kutokana na kuathiriwa na PERSISTENCE OF VISION na hapo tunapata psychological effect called BETA MOVEMENT sina tafsiri sa hihi ya maneno haya ila unachopaswa kujua filamu ni muunganiko wa picha moja na nyingine sasa tunapoangalia filamu muunganiko huu wa picha moja mpaka nyingine unauona katika kasi ya ajabu kiwango cha sekunde ndiyo tupata picha zinazotembea kutokana na kuathiriwa na kasi hiyo ya hizo picha.
Historia ya filamu imepitia hatua mbalimbali kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Miaka ya 1600's maonyesho ya jukwaani(theaters play) kwa wakati huo yalishamiri sana barani ulaya maonyesho haya yalijumuisha matumizi ya script,casts(wasanii),setting designe,stage direction(directing), costumes and make up (marembo sanaa) na mengineyo ambayo hata kwa sasa katika hatua ya uzalishaji nilazima ili filamu ikamilike yatumiwe.
Katikati ya miaka ya 1600's mpaka 1800's ugunduzi wa kifaa mfano wa camera uliweza kuchukua mwanga wa picha na kupelekea picha zinazotembea lakini kifaa hicho kilishindwa kurekodi picha hizo na kuzihifadhi.
Miaka ya 1800's mpaka 1900's camera aina hand crane ilivumbuliwa camera hii ilikuwa na uwezo wa kurekodi picha na kuhifadhiwa.
ikumbukwe kuwa kwa wakati huo kipengele cha uhariri(editing) hakikuwepo na filamu zilikuwa fupi sana kuonyeshwa.
Miaka ya 1900's mpaka 1920's filamu ziliweza kurekodiwa lakini bila ya mazungumzo ya wasanii(dialogue) kilichoweza kufanyika ni kuambatanisha picha pamoja na sauti za muziki mara nyingi mziki wa jazz ulitumika kipindi hichi kilijulikana kama LESS TALKIES(filamu bila mazungumzo) tazama filamu za vichekesho za Charlie Chaplin.
Kipindi hiki cha mwaka 1920 ulaya ambayo ilitamba sana katika uzalishaji wa filamu iliathiriwa vibaya mno na vita kuu ya kwanza ya dunia kwa maana hiyo soko la uzalishaji filamu likahamia Holly wood Center Marekani katika jiji la Los Angeles California na hapo kukaibuka kampuni kubwa za uzalishaji filamu kama Warner Bros,MGM na kampuni nyinginezo zilizoleta ushindani mkubwa katika soko la dunia.
Katikati ya mwaka 1920's ugunduzi mwingine ulifanyika nao ni kuambatanisha picha zinazotembea pamoja na mazungumzo(dialogue) kipindi hiki kilijulikana kama (THE TALKIES)
Tangia mwaka 1920 filamu zilendelea kurekodiwa bila ya rangi mpaka mwanzoni mwa miaka ya sitini mpaka katikati hivi ndiyo hapo kwa mara ya kwanza picha hizi zinazotembea ziliambatanishwa na kurekodiwa katika rangi filamu zikapata muonekano wa rangi kipindi hiki waliibuka waigizaji maarufu kama Stevene Mcqueen,James Belushi,Bruce Lee, filamu za kwanza za James Bond zilichezwa, kina Danny Groover wakaibuka kipindi chote hichi filamu zilizalishwa na makampuni makubwa kama MGM na Warner Bros.
Kuanzia mwaka wa 1960's mpaka 1980's nguvu ya kampuni hizi kuzalisha filamu ulielekea kufikia kikomo na ndiyo hapo kukaibuka kwa watengeneza filamu binafsi independent film makers(indie films) na hapa taratibu majumba ya sinema yakaanza kupungua huko ulaya kwani filamu zilizalishwa kwa watazamaji wa nyumbani(home made user) kukaibuka kwa VHS tape ikumbukwe Tanzania majumba ya sinema kama the Avalon,Empire ndiyo yalishamiri mpaka katikatia miaka ya tisini ndiyo VHS tape kwa ajili ya watazamaji wa nyumbani zilipoibuka pengine kutokana na kuingia katika uchumi huria.
Miaka ya 1990's mpaka 2000's filamu zilizojulikana kama BLOCK BUSTERS zilishamiri wachezaji filamu maarufu kina Sylivester Stalone na Rambo,Jean Claude Van Damme na Blood Sport.
Katika miaka ya 2000's na kuendelea filamu zikazalishwa mfumo mpya huko ulaya ujulikana kama 3D teknoloji ukitazama filamu katika mfumo huu unajiona mtazamaji kama sehemu ya tukio la hadithi katika filamu unayotazama mfano mtu akiwa anaungua unahisi na kupata hisia zote(emotion effects).
HATUA ZA UZALISHAJI FILAMU
Ili filamu iweze kukamilika inapitia hatua nne muhimu kwa mujibu wa mtindo wa utengenezaji filamu wa kimarekani Holly Wood style)
1.Development ....hatua hii mzalisha filamu anapata wazo la hadithi ya filamu(idea) na kuanza kuifanyia kazi wazo lake
2. Pre production ...hatua hii mzalisha filamu baada ya kupata wazo anaandaa Script ya hadithi ya filamu yake na kwa mujibu wa wataalamu script ni muongozo wa hadithi ambao unamuongoza director na wasanii pamoja na muongozaji wa kupiga picha (D.O.P) Director of Photograph jinsi picha zitakavyochukuliwa, script au Screen play kwa jina jingine inabeba hadithi nzima ya filamu picha katika maandishi script inakuwa na Scene heading,dialogue na action mfano:
SCENE HEADING:
EXT.(NJE) NYUMBANI KWA HARITH-(WAKATI)DAY
ACTION: (TUKIO)
Harith akiwa amelala anajigeuza upande mmoja wa kitanda mpaka mnwingine mara mlango unafunguliwa anaingia mwanamke aliyejifunga kilemba
DIALOGUE:
MWANAMKE
Mpenzi amka basi
dear jamani amka
katika hatua hii muandaaji ataandaa Story Board(michoro ya hadithi),atatafuta wasanii na kampuni ya kupiga picha,atatambua crew(kikundi cha ufundi) kwa ajili ya kupiga picha na watu ataoshirikiana nao
kama watu wa marembo(make up), mtu wa location n.k
3.PRODUCTION hatua hii maandalizi ya kupiga picha yanaanza hapa atakuwepo director(muongozaji), msaidizi wake Assistant director, muongozaji mpiga picha (D.O.P), katika hatua hii shughuli nzima inakuwa chini ya Director baada ya upigaji picha hatua inayofuata ni uhariri(editing)
4.Distribution.....hatua hii ndiyo usambazaji hufanyika mambo ya masoko(marketing) huchkua nafasi yake
Hatua hizi zote nne kwa mujibu wa wataalamu huchukua miaka mitatu kufanyika tazama watengenezaji wa hapa nyumba katika mwezi msanii anatoa filamu si chini ya moja filamumbili tatu sasa unajiuliza anashuti saa ngapi na kuhariri muda gani ndiyo maana filamu zetu zinakuwa na makosa mengi muandaji anakimbizana na muda alimradi amalize kupiga picha, wenzetu wana mpaka watu wa dialogue(dialogue coach master) msanii anafundishwa jinsi ya kutamka maneno kama hadithi inahusu lafudhi watu wa lafudhi wanamsaidia katika utamkaji wa maneno.
Filamu ina uwanja mpana sana wa kujifunza na ina mambo mengi ya kiufundi lazima kujfunza mambo hayo na yana patikana bure katika mtandao, unaweza kujifunza jinsi ya uandishi wa script,ukasoma production team n.k
Nakushauri uanze kujifunza uandishiwa script na hadithi ya filamu(film treatment), usome production team inakuwaje, ujue shoti mbalimbali za filamu tumia search engine google kujifunza
Kwanza nikupongeze sana bwana Harithi kwa makala yako inayovutia na kuelimisha. Binafsi nimefurahishwa sana na jinsi ulivyojikita katika uwanja wa filamu nikizingatia taaluma yako haikuwa huko. Japo mambo mengi uloyaeleza hapa yanapatikana katika mtandao, ni jambo la kuvutia kuyaona kwenye lugha ya kiswahili japo si yote.
ReplyDeleteNachotaka kusisitiza tu ni jinsi gani tutatumia hiyo historia ya filamu (iliyotoka Ulaya na Marekani)kuleta mabadiliko ya filamu nchini.
Inasikitisha sana kuona wasanii wa filamu ni walewale (fixed characters) utadhani filamu zote zina lengo moja.
Kwa wenzetu waliotuletea hiyo historia, mtu wa kawaida anaweza kuombwa kushiriki kwenye filamu ili mradi ana sifa zinazoendana na kisa cha filamu hiyo (hata kama si msanii), atapewa mafunzo. kwa vile hapa Bongo watu wanaigiza filamu kwa dhamira mbalimbali, si rahisi mtu kumtafuta (ordinary citizen) ashiriki filamu yake kwa vile filamu ni mahali pa kuuza sura. Hili linatuangusha sana mwishowe unakuta mtu ana kitambi, amenawili halafu anacheza nafasi ya maskini asiyejiweza!!