Tuesday, May 1, 2012

WAKATI NI HUU KWA TANZANIA KUWA NA TUNZO ZA FILAMU ZENYE SURA KITAIFA

Namshukuru mungu na afya njema nikiendeleza gurudumu la maisha mapambano yanaendelea ni ukweli usiopinga kwa sasa pamoja na soko la filamu kuwa kubwa hii ikithibitishwa kutokana na uzalishaji uliongezeka wa filamu hizo Tanzania katika sanaa hii maridhawa tumekosa kitu cha kutuunganisha wadau wote wa filamu kubwa ya yote ni tuzo za filamu zilizomakinika na zenye sura kitaifa. kwa upande mwingine wa sanaa mfano katika muziki kuna tuzo tunazijua tuzo kubwa kabisa kupitia udhamini wa kampuni ya bia Kilimanjaro zijulikanazo kwa jina la Kilimanjaro music awards ingawa kumekuwa na malalamiko ya hapa na pale kuhusu tuzo hizo kwa mwaka huu ikiwemo na kujitoa kwa baadhi ya wasanii hilo si haba tuzo hizo zipo na zimeendelea kutolewa mwaka hadi mwaka. Kwa nchi za magharibi Mfano Marekani wao wanatunzo mbalimbali za filamu kubwa na tuzo lijulikanalo ni Oscara film awards tuzo hii imekuwepo kwa miaka mingi na inaheshima kubwa katika tansia ya filamu Marekani. Kwa Tanzania zipo tuzo mbalimbali ambazo bado hazina taswira ya kitaifa mfano Zanzibar Internationa film festival awards ambapo mataifa mbalimbali ya afrika na wadau wa filamu hukutana na filamu kutoka katika mataifa hayo huonyeshwa tuzo hizi zimegawanyika katika vipengele mbalimbali kubwa linalozingatiwa ni ubora wa filamu husika katika kipengele cha uzalisha(production),ubora wa matumizi ya upigaji picha na hadithi nzima ya filamu husika katika tamaduni za kiafrika kipengele cha kwanza cha tuzo hizo kinajulikana kwa jina la Golden Dhow award ambapo kwa mwaka jana tuzo hiyo ilienda kwa Bob Nyanja kutoka Kenya na filamu yake ya The rugged priest, kipengele kingine ni cha tuzo hizo ni Silver Dhow ambapo kimeenda kwa Nathan Collett kutoka Kenya na filamu yake iitwayo Togetherness Supreme. Kwa upande wa Tanzania Jokate Mwegelo alishinda kipengele cha Best Actress na kipengele cha muongozaji bora kilienda kwa muongozaji Jordan Riber kwa upande wa kipengele cha Documentary film filamu zinazoakisi maisha halisi kwa mtindo wa masimulizi bila ya kuongeza utundu wa editors Golden Dhow kilienda kwa Penelope Machimbi raia wa Zambia na filamu yake The hidden Truth wakati huo kipengele cha Silver Dhow kilienda kwa Riaan Hendricks kutoka Soth Afrika na filamu yake ya The Last Voyage. kwa upande wa filamu bora ya afrika mashariki kipengele cha Best East African Film kilienda kwa Zalalem Woldemariam na filamu ya Zalalem kutoka Ethiopia, kipengele cha Best Short film kimeenda kwa Mahay Petrossian na Amir Toodehrossa. Katika kipengele cha Swahili Awards Best feature film kilienda kwa Ray of hope kwa muandaaji Sajni Srivastava Best Actor imeenda kwa Jacob Stephen na filamu ya Senior Bachelor. Licha ya kuwepo tuzo hii Zanzibar film festival ambayo bado kama nilivyosema hazina taswira ya kitaifa kama zilivyo tuzo nyingine katika mataifa makubwa kama marekani Hollywood,India Bollywood na Nollywood nchini Nigeria ni busara Basata na shirikisho la filamu Tanzania TAFF kuliona hili na kulifanyia kazi jamani tansia hii inamapato makubwa endapo serikali ikaweka mkono wake katika kusimamia kazi za wasanii ikiwemo pamoja na kutunga sheria kali kwa wale wanarudufu kazi za wasanii kinyume na sheria(pirates) na kuziingiza sokoni. Serikali imetoa ahadi ya kupambana na wizi wa kazi za wasanii kupitia waziri wa habari na michezo Mheshimiwa Emanuel Nchimbi ilitoa ahadi hiyo katika mazishi ya msanii nguli wa filamu marehemu Steven Charles Kusekwa Kanumba wadau tumeisikia ahadi hiyo na tunasubiri utekelezaji wake ukamilike. Tansia hii itaendelea kuwepo endapo wadau wa sanaa hii tutashirikiana na kuondoa makundi ambayo hayana tija TAFF shirikianeni na Basata kutuunganisha wadau wa filamu kwa kufanya semina mbalimbali.

Thursday, March 8, 2012

WAKATI NI HUU KWA TANZANIA KUWA NA TUZO ZA FILAMU

Namshukuru mungu na afya njema nikiendeleza gurudumu la maisha mapambano yanaendelea ni ukweli usiopinga kwa sasa pamoja na soko la filamu kuwa kubwa hii ikithibitishwa kutokana na uzalishaji uliongezeka wa filamu hizo Tanzania katika sanaa hii maridhawa tumekosa kitu cha kutuunganisha wadau wote wa filamu kubwa ya yote ni tuzo za filamu zilizomakinika.

kwa upande mwingine wa sanaa mfano katika muziki kuna tuzo tunazijua tuzo kubwa kabisa kupitia udhamini wa kampuni ya bia Kilimanjaro zijulikanazo kwa jina la Kilimanjaro music awards ingwa kum ekuwa na malalamiko ya hapa na pale kuhusu tuzo hizo kwa mwaka huu ikiwemo na kujitoa kwa baadhi ya wasanii hilo si haba tuzo hizo zipo na zimeendelea kutolewa mwaka hadi mwaka.

Kwa nchi za magharibi Mfano Marekani wao wanatunzo mbalimbali za filamu kubwa na tuzo lijulikana ni Oscara film awards tuzo hii imekuwepo kwa miaka mingi na inaheshima kubwa katika tansia ya filamu Marekani.

Kwa Tanzania zipo tuzo mfano Zanzibar Internationa film festival awards ambapo mataifa mbalimbali ya afrika na wadau wa filamu hukutana na filamu kutoka katika mataifa hayo huonyeshwa tuzo hizi zimegawanyika katika vipengele mbalimbali kubwa linalozingatiwa ni ubora wa filamu husika katika kipengele cha uzalisha(production),ubowra wa matumizi ya upigaji picha na hadithi nzima ya filamu husika katika tamaduni za kiafrika kipengele cha kwanza cha tuzo hizo kinajulikana kwa jina la Golden Dhow award ambapo kwa mwaka jana tuzo hiyo ilienda kwa Bob Nyanja kutoka Kenya na filamu yake ya The rugged priest, kipengele kingine ni cha tuzo hizo ni Silver Dhow ambapo kimeenda kwa Nathan Collett kutoka Kenya na filamu yake itwayo Togetherness Supreme.

Kwa upande wa Tanzania Jokate Mwegelo alishinda kipengele cha Best Actress na kipengele cha muongozaji bora kilienda kwa muongozaji Jordan Riber kwa upande wa kipengele cha Documentary film filamu zinazoakisi maisha halisi kwa mtindo wa masimulizi bila ya kuongeza utundu wa editors Golden Dhow kilienda kwa Penelope Machimbi raia wa Zambia na filamu yake The hidden Truth wakati huo kipengele cha Silver Dhow kilienda kwa Riaan Hendricks kutoka Soth Afrika na filamu yake ya The Last Voyage.

kwa upande wa filamu bora ya afrika mashariki kipengele cha Best East African Film kilienda kwa Zalalem Woldemariam na filamu ya Zalalem kutoka Ethiopia, kipengele cha Best Short film kimeenda kwa Mahay Petrossian na Amir Toodehrossa.

Katika kipengele cha Swahili Awards Best feature film kilienda kwa Ray of hope kwa muandaaji Sajni Srivastava Best Actor imeenda kwa Jacob Stephen na filamu ya Senior Bachelor.

Hatuna budi wadau wote wa filamu kuwa na kitu kitakachotuunganisha kitaifa moja ya yote ni tuzo za filamu kwa Tanzania zisizo na ubabaishaji na zinazozingatia ubora.

Thursday, March 1, 2012

HILI LA ADA ZA UANDAAJI FILAMU LIANGALIWE UPYA NA BODI YA FILAMU TANZANIA

Namshukuru mola kwa kunijaalia afya njema mpaka wakati huu kila binaadamu anamatarajio yake katika maisha yake lakini kubwa ya yote ni afya njema mungu mjaalie dada yangu aendelee kupata ahueni.

Mwaka jana mwezi wa kumi niliandika makala kuhusu sanaa ya filamu Tanzania na utitiri wa uzalishaji wa filamu kila kukicha bila ya kuzingatia ubora wa kazi hizo niukweli usio pingika kazi hizo hazina ubora kuanzia katika uandishi wa hadithi za filamu(story) katika miswaada(script) mpaka katika uzalishaji mzima (production).

Kilichoniua nguvu mwaka huo mwaka jana bodi ya filamu na michezo ya kuigiza ikaingiza kanuni sijui waigizaji wenyewe na wataarishaji filamu walishirikishwa,kanuni hizi moja ya kanuni ni hii 1. Wataarishaji filamu kuomba kibali cha kuandaa filamu kwa ada ya laki tano 500,000Tsh fedha za kitanzania mwenzi mmoja kabla ya kuanza kuandaliwa kwa filamu 2.Baada ya kibali upitiaji wa mswaada kwa ada ya 60,000tsh kutegemea na urefu wa hadithi kwa saa, sababu eti ni swala la uzingatiaji wa maadili walikuwa wapi wakati wote huo kanuni kama hizi zinaletwa sasa wakati huu kukiwa na utitiri wa filamu, ni ukweli usio pingika soko limekubali kanuni hizi hazilengi filamu za kitanzania hata zile za nje pia kwa upande wa uingizwaji wa filamu hizo nchini.

Kanuni hizi kwa upande mmoja hazilengi kumsaidia mwananchi wa kawaida ambaye kwa mapenzi ya dhati amejiingiza katika ujasiriamali huu wa uandaaji wa filamu ada ni kubwa mnoo bodi ya filamu waliangalie hiloo huenda ndiyo ukawa mwisho wa filamu za kitanzania ingawa katika upande wa pili ikasaidia katika kulinda maadili cha muhimu kanuni hizo zilenge pande zote mbili.

Wazo langu moja serikali na bodi ya filamu na michezo ya kuigiza Tanzania ipitie upya kanuni hizo na kupunguza ada ya uandaaji hailengi kumsaidia mjasiriamali wa kawaida mwenye ujuzi na sanaa hii.

Mbili serikali na bodi ya michezo ya kuigiza itumie nguvu nyingi katika kulinda kazi hizi za sanaa zisihujumiwe na watu wachache wasiojua uchungu na adha tuzipatazo wataarishaji filamu na waongozaji gharama ni kubwa katika kutafuta location(maeneo ya upigaji picha), waigizaji wenyewe,kampuni ya upigaji picha,usafiri na hata kuweka wasanii kambini ni gharama mnoo.

Monday, November 21, 2011

WIZI HUU WA KAZI ZA SANAA MPAKA LINI?

Habari zenu bana? mi niko poa sana nilishtushwa na taarifa katika televisheni ya channel ten mwanamama wa shoka Asha Baraka akilalamikia uchakachuaji uliyofanywa katika albamu mpya ya twanga.Kiukweli inauma unafanya kazi yako kabla haijatoka wajanja washapiga kopi mzigo uko mtaani dah wizi huu utaendelea hivi mpaka lini? kuna haja ya serikali kuingilia kati kwa mikakati iliyo bora ilikuzibiti wizi huu iwe kwa kutungwa sheria kali kuboresha miundo mbinu ya usambazaji na kuwe na bodi maalum iliyoundwa na serikali kama ilivyo mamlaka ya usafirishaji Sumatra na chombo hiki kifanye kazi yake chini ya sheria maalum.

Katika filamu hali ni ile ile wiziwizi msanii au muandaji wa filamu unaumiza kichwa kwa kuandaa filamu nzuri unaipeleka sokoni wajanja tayari washapiga kopi zao basata iko wapi? bodi ya filamu hawana angalau mkakati wa kudhibiti hali hii? jasho la wasanii linavuja bure.

Sanaa ni ajira kwa sasa serikali ilitazame hili kwani pi wao watanufaika kutokana na mapato mengi watakayopata kupitia kodi wizi wanamna hii unapoteza mapato mengi kwa serikali na tansia nzima ya sanaa ikiwemo msanii mwenyewe.

Sunday, October 30, 2011

Hivi ni bora filamu au filamu bora bongo movies?

Namshukuru mola kwa kuwa nina afya njema mipango yangu ya kuandaa filamu inakwenda vizuri jicho langu leo katika filamu nitaangazia ubora wa uzalishaji wa filamu na tamthilia za hapa nyumbani.

Miaka ya hivi karibuni idadi ya filamu na uzalishaji wake umeongezeka mara dufu ya kipindi cha nyuma hili ni uthibitisho kwamba filamu Tanzania ni biashara kubwa na ina soko sasa je najiuliza ni bora filamu au filamu bora?

Tukianzia na hili la uzalishaji kama nilivyosema hapo mwanzo idadi ya filamu zinazozalishwa hapa nchini Tanzania umeongezeka maradufu lakini cha kusikitisha uzalishaji huu hauzingatii ubora wa filamu nasema hivyo mfano msanii au kampuni kwa mwezi mmoja inatoa filamu tano kwa msanii mmoja sasa unajiuliza hadithi inatungwa saa ngapi au hiyo script(screen play) inarekebishwa muda gani mpaka ikapatikana script sahihi(final draft).

Swala jingine uzalishaji wenyewe je ni viwango vinavyotakiwa? jibu nalo lipata ni hapana uzalishaji hauzingatii ubora kwa mfano jioni moja nilibahatika kuangalia filamu moja wapo jina sitolitaja lakini cha kusikitisha nilichokiona katika filamu ile ni uzalishaji mbovu tukianzia katika upande wa sauti, sauti za waigizaji zilikuwa hazisikiki kabisa nilichokuwa nasikia ni sauti za nje ya dialogue(sound track) basi sasa unajiuliza walitumia vinasa sauti vya aina gani? kurekodi pili waigizaji baadhi walichemka nashindwa kuelewa director hakuliona mfano muigizaji anahadithia tukio la huzuni la kufiwa na mtu wake wa karibu kweli anaonyesha huzuni lakini kutoka hapo kwenye huzuni sasa ghafla anaanza kucheka na mwenzake wakati huo huo walikuwa katika huzuni hao hivi ni rahisi kweli kihivyo hisia ya huzuni kubebwa ghafla na furaha ikizingatia huzuni yenyewe inahusisha kifo cha mtu wa karibu kabisa...kazi ipo

Na hili jingine ni la kusikitisha na kufedhehesha jamani hata maongezi(dialogue) katika filamu zetu kwa lugha yetu tunashindwa kweli? hili nililiona katika tamthilia moja wapo inayorushwa na kituo kikubwa cha televisheni hapa nchini katika hadithi ya tamthilia ile kulikuwa na tukio mauaji na kama kawaida askari walikuwa katika tukio lile kwa ajili ya uchunguzi cha kuchekesha sasa mmoja wapo wa askari wale akawa anaongea kupitia simu ya upepo(radio call) maongezi yake yalianza hivi...."AFANDE KUNA MAUAJI YA MAITI......? niliposikia nikashtuka na kupigwa na butwaa hivi hawa waongozaji,wasanii wenyewe na hata hayo makampuni wataendelea mpaka lini kushusha hadhi yetu ya filamu hapa Tanzania na kuturudisha nyuma kweli tuna hatua ndefu sana kufikia mahala tunapopataka.

Wakati nipo chuo kikuu cha Dar es salaam nilisoma kozi moja ya African Cinema katika kozi ile kulikuwa na kipengelee cha kupitia filamu za kiafrika na kuzifanyia uchambuzi kwa kweli nilifurahishwa na filamu ya Harusi ya Mariam filamu ambayo imechezwa hasa katika mandhari ya vijijini Tanzania wakiwemo waigizaji maarufu kama mama Tekla Mjata ukisikiliza maongezi(dialogue) kweli unasikia hasa lafudhi za watu wa eneo lile sikumbuki ilikuwa ni sehemu gani ya kijiji na hata sauti zilikuwa katika ubora wake ikumbukwe ni kipindi cha nyuma kidogo miaka ya kati ya sitini na sabini hivi wakati ambao vifaa vya kurekodi si vya kisasa kama ilivyo sasa

Ombi langu bodi ya filamu Tanzania na Basata kuna haja ya wahusika kutazama utitiri wa filamu hizi unaotokakila kukicha bila kuzingatia ubora na kuturudisha nyuma hatua kumi badala ya kusonga mbele....

Thursday, October 6, 2011

Bongo movies kwa hili tutafika kweli?

Nimesikitishwa sana nilipokuwa nasoma baadhi ya magazeti yakiwa na taarifa kwamba mwanadada Anti Ezekiel amesimamishwa kucheza filamu kwa sababu zisizojulikana naisema hivyo kutokana na kile nilichokisoma katika magazeti pendwa(udaku) je nalo hili ni zengwe au...swali nililojiuliza mara baada ya taarifa hizo ni nani mwenye uwezo wa kumfungia msanii wa filamu ni bongo movie au ni shirikisho la wasanii ikumbukwe kwa viwango tulivyo navyo napata wasiwasi sana na tansia hii ya filamu inapokwenda hatujafikia viwango hata vya Nollywood nchini Nigeria tayari wamejitokeza miungu watu katika tansia hii ambao wanaweza kuchagua ni msanii gani acheze filamu nani asicheze na inajulikana kabisa bila ya wasanii fulani filamu haiuzi

Kwa hili ni changamoto kubwa katika fani hii hatuwezi kuwa na wasanii wachache ambao bila wao filamu haiuzi ili tuweze kuendelea na kufika tunapotaka lazima tujifunze kupitia wenzetu mfano Nigeria ukiachana na Rmsey Noah kuna kina Emeka Ike,Desmond Eliot,Zak Orgi na sasa Nchini Ghana Van Vicker lazima kuwe na ushindani kwa wasanii na hata makampuni ya uzaishaji mfano sasa kuna Step entertainment ni muda muafaka kujitokeza kwa makampuni mengine yatakayoleta ushindani bila ya kubagua wasanii walete ushindani kwa filamu bora nasiyo bora filamu kama ilivyosasa...

Filamu za bongo na majina ya kiingereza ni ulimbukeni ama? tujadili

Mambo vipi? nashukuru kama uko poa kwa wapenzi wa bongo movies ningependa tujadili jambo katika tansia yetu hii ya filamu nalo si jingine bali ni kuhusu film title au jina linalobeba filamu imekuwa nimazoea kwa sasa filamu nyingi za bongo zinabeba majina ya kiingereza we unalionaje hili naomba utoe mchango wako vipi iko poa kutumia majina ya kiingereza na wakati huo kilichomo ndani ya filamu hizo ni maongezi(dialogue) kwa lugha ya kiswahili je hili ni ulimbukeni au? mchango wako