Thursday, December 30, 2010

Je tunawaenzi vpi wapigania uhuru wetu?

Mwezi wa  sita katikati ya  mwaka 2010  nilitembelea  Dodoma  kabla ya  hapo nilipata kusikia  stori mbalimbali kuhusu Dodoma  kwamba ni kukame hakuvutii kuna vumbi na  vitu vingine kama  hivyo lakini nilipofika mahala hapo nilivutiwa na jinsi mkoa huu wa  Dodoma unavyovutia, na unaonyesha ni  jinsi  gani unakuwa  kwa  kasi sana, katikati ya  mji wa Dodoma nilivutiwa na  bustani iliyopewa  jina lampigania uhuru wa  nchi yetu Mwalim  Nyerere yaani nyerere  Skweya  eneo  hilo linavutia  kwa bustani nzuri na sanam ya  muasisi wa  taifa letu, tumezoea kusikia majina kama bibi Titi Mohammed na  barabara ya Bibi Titi, Je vipi kina kinjeketile mzee  na mganga aliyehamasisha vita ya kumn'goa mjerumani wakati ule wa  vita  ya majimaji mwaka 1905 mpaka 1907 kuna mmatumbi anayejulikana kwa jina la Abdallah  Manyanya ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuuwa katika vita ya majimaji huko lindi Kilwa katika kijiji cha  Kibata ukiiangalia historia ya  Tanganyika wakati  huu  Tanzania ukombozi wake ulianzia siku  nyingi miaka ya 1800,s sana wa afrika wa Tanganyika kwa wakati  huo tulikataa  uvamizi wa watu kutoka mataifa ya  ulaya,Asia na mashariki ya mbali ikiwemo wa  Arab, tawala hizi ndio zilikuwa vamizi za  kwanza katika ardhi ya Tanganyika kama ilivyojulikana kwa wakati huo kabla ya mwaka 1961.Historia inatuambia  wamatumbi,wa hehe, wanyamwezi  na  makabila mengine kusini mwa Tanganyika,Tanzania walikataa  uonevu na udhalimu ulioletwa na  vamizi hizi mfano wa Jerumani baadaye waingereza, kulikuwa kuna waarabu walikaa miji ya Kilwa, Bagamoyo hawa waliendesha shughuli ya  Utumwa, kwa  hiyo harakati za  mwanzo kabisa zilikuwa maalum kwa ajili ya kupambana na  vamizi hizi ambazo zilileta utumwa,zilichukuwa ardhi zetu na zilitumikisha kwa  nguvu na uonevu wa Tanganyika walifanyisha kazi katika mashamba makubwa na kulipwa ujira mdogo,ila baada ya 1800's na mwanzoni mwa miaka ya  1900's harakati za mwa  afrika na watu wa |Tanganyika ilikuwa ni kupambana na Ukoloni wa  Wajerumani na  Baadaye Waingereza.Kuna haja tukaiangalia historia yetu kwa  Mapana ili kuepusha kupotea kwa historia hizi adhimu na  adimu.

No comments:

Post a Comment