Friday, January 28, 2011

CHUO KIKUU DAR ES SALAAM KIMEONYESHA NJIA KATIKA MJADALA WA KATIBA

Wiki kama mbili zilizopita hivi kulikuwa na Kongamano la Katiba wasemaji wakuu walikuwa Profesa Shivji na Nguli wa habari Jenerali Ulimwengu mjadala uliokuwa unarushwa moja kwa moja na Kituo cha televisheni cha ITV,mjadala huo uliijadili kihistoria katiba ya Tanzania na mabadiliko yake toka mwaka 1961 mpaka 1977 ilipopatikana katiba ya leo,yalielezwa mengi na wanazuoni kina Shivji na Jenerali na haja ya kuhitaji katiba mpya dhima kuu ilikuwa hoja ya katiba mpya na Ushirikishwaji wa wananchi,mapendekezo mbalimbali yaliongelewa kupekelea mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya.
  Wazo langu kwanza napenda nikipongeze chuo cha Dar es salaam na Uongozi wa Udasa kwa kuandaa kongamano hilo ila kubwa ya yote chombo cha habari cha ITV kwa kurusha moja kwa moja matangazo ya kongamano hilo la katiba, ningependa vyuo Vikuu vingine viige mfano huu wa chuo Kikuu Dar es salaam pamoja na vyombo vingine vya habari vingine vifuate mfano wa ITV kurusha matangazo hayo.
    Elimu ya katiba yetu na hii mpya tunayotarajia kuundwa kwake ipelekwe kwa wananchi hasa mikoani na  vijijini serikali za vijiji waitishe mikutano kujadili uundwaji wa katiba mpya na wananchi wajadili ni vipi wangependa katiba hiyo ishirikishe wananchi wake eidha kwa kura ya maoni swala la rasilimali za taifa lijadiliwe na vpi katiba hii itampa mamlaka mwananchi wakawaida kulinda rasilimali zake,ikiwemo pia na utunzaji wa rasilimali hizo kutokana na uharibifu wa mazingira.
    Elimu  hii ipelekwe mashuleni  na vyuoni kuwa na makongamano kama hilo la UDSM, wanafunzi watoe mawazo yao, na waeleze uelewa wao  juu ya katiba mpya na ni vipi wangependa elimu ya Tanzania ipewe kipaumbele gani katika katiba hii .
     Wafanyakazi wa sekta rasmi na binafsi nao wajadili swala la katiba kwa mfumo wa kongamano kama hilo la UDSM.
       KATIBA MPYA MCHAKATO NDIO HUU UMEANZA HEKO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM, ITV  HONGERENI  SHIVJI NA GENERALI ULIMWENGU,UDASA WANAFUNZI ,WAZIRI KOMBANI,WANASIASA NA WAUDHURIAJI WOTE WA KONGAMANO HILOLA KATIBA

No comments:

Post a Comment