Sunday, February 6, 2011

YALIYOTOKEA MISRI(EGYPT( NI MFUNZO KWA TAWALA ZA KIAFRIKA

Kile tulichokiona Tunisia na leo hii tunaendelea kukishuhudia Misri ni funzo kwa tawala za Africa  ambazo zimeendelea kuwa madarakani kwa muda mrefu huku wakiendela kujilimbikizia mali pasipo kujali maisha ya wananchi wake wanaoishi maisha ya hali ya chini mno.

   Wakati nipo chuo kiuu Dar es salaam nilipata kusoma kozi moja ya Historia ambayo inaeleze ni jinsi gan i  mapinduzi kwa nchi za Africa yanavyochochewa na tawala mbovu zisizojali maisha ya wananchi wengi, kwa mfano nilipata kusoma nchi kama Misri ambayo ilitawaliwa kwa muda wa takribani miaka 2000's na mataifa kutoka nchi za magharibi mfano Uingereza katika miaka ya 1890's, walikuwepo kabla ya hapo tawala kama za Turkish Rule  Waturuki wanaonekana kama watu kutoka Ulaya na uarabuni.



        Mapinduzi ya Misri 1952 chini ya mwanamapinduzi asiyesahaulika misri Gamal Abdil Nasser yalilenga kukikomboa Misri kutoka katika tawala ambazo hazikujali maisha ya wananchi wakawaida wa Misri hali kama kutokuwa na ajira,umaskini ni vitu ambavyo tunaviona leo hii wananchi wa Misri wakilalamikia utawala wa Hosni Mubarak umeshindwa kuvipatia ufumbuzi , hapa ndio tunaona nguvu ya wananchi inapotumika kudai haki na kupiga kelele kwamba Rais Hosni Mubarak ha na tena nafasi kwa wananchi wa Misri amboa wanahitaji mabaliko ya kiuchumi na kijamii hili ni funzo kwa nchi yetu Tanzania na nchi nyingine za Afrika kwamba viongozi wetu wasijisahau katika tawala zao.

No comments:

Post a Comment